MANCHESTER UNITED KUVUNJA BENKI KWA GARETH BALE …yajiandaa kumpa mshahara wa pauni 300,000


MANCHESTER UNITED KUVUNJA BENKI KWA GARETH BALE …yajiandaa kumpa mshahara wa pauni 300,000

Gareth Bale missed Real Madrid's Champions League                  Group B match against Liverpool due to a buttock injury

MANCHESTER United imepiga hatua kubwa mbele katika harakati zake za kutaka kumpeleka Old Trafford Gareth Bale baada ya Real Madrid kuripotiwa kuwa tayari kumuweka sokoni.

Klabu hiyo ya England inayojipanga upya, inaaminika kumfanya Bale kuwa lengo lao namba moja katika usajili ujao wa Januari, huku ikiwa tayari kumlipa mshahara wa pauni 300,000 kwa wiki.

Taarifa kutoka Hispania zimedai kuwa kocha Carlo Ancelotti yuko radhi kumwachia Bale aondoke Bernabeu, akielezwa kwamba si chaguo lake kwenye katika kikosi cha kwanza kufuatia kiwango kizuri kinachooneshwa na Isco.

Madrid inaelezwa kutaka pauni milioni 90 iweze kumwachia Bale, kiasi ambacho United iko tayari kulipa.



Comments