Makocha                35 wameteuliwa kushiriki kozi ya ukocha ya Leseni C ya                Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) itakayofanyika                mjini Morogoro kuanzia Novemba 5 hadi 19 mwaka huu.
        Kozi hiyo itaendeshwa na Mkufunzi wa                  CAF, Sunday Kayuni na itafanyikia Mchikichini College                  ambapo washiriki wote wanatakiwa kuwasilisha vyeti vyao                  vya ukocha vya ngazi ya Kati (Intermediate) pamoja na                  vyeti vya kitaaluma vya elimu ya sekondari (academic).
        Washiriki wa kozi hiyo ni Abdulmaliki                  Nemes (Airport FC), Ahmed Haule (Kilimanjaro Talented                  Youth Sports Centre), Ally Jangalu (Moro Kids), Amri                  Saidi (Mwadui FC), Athuman Kambi (Morogoro), Charles                  Mwakambaya (Burkina Faso FC),  Damian Mussa (Alliance                  One) na Daudi Sichinga (Kasulu United).
        Denis Maneva (Shule ya Msingi Logo),                  Edgar Juvenary (JUT- Mlale), Hamisi Mangolosho (Shule ya                  Msingi Mtimbwilimbwili), Henry Ngondo (Chalinze                  Academy), Issa Hamisi (Polisi Kilimanjaro), Jumanne                  Chale (Dar es Salaam), Kizito Mbano (Masasi Alliance),                  Martin Saanya (Magereza Morogoro) na Masoud Gumbwa                  (Sokoine University Academy).
        Mbwana Makata (Oljoro JKT), Mrage                  Kabange (Kagera Sugar), Muhibu Muhibu (Stand United FC),                  Nsubuga Solomon (Kishoto FC), Nyamtimba Muga (Kizuka                  Secondary), Oscar Mirambo (Makongo), Rashid Abdallah                  (Tech Fort Academy), Renatus Shija (Rhino Rangers),                  Safari Nyerere (Elimu Sports Academy) na Said Lyakuka                  (Kizuka Stars).
        Simeon Mwesa (Mtibwa Sugar U20),                  Simon Shija (Tabora), Suleiman Mtungwe (Ruvu Shooting),                  Swalehe Allawi Abdul (Alliance Academy), Yasin Bashiri                  (Kick Off Sports Academy) na Zuberi Katwila (Mtibwa                  Sugar).
        Wakati huo huo, kutakuwa na kozi ya                  wiki mbili ya ukocha ya ngazi ya Kati (Intermediate)                  itakayofanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Desemba 29                  mwaka huu.
        Makocha wote wanaotaka kushiriki kozi                  hiyo wanatakiwa kutuma maombi katika Chama cha Makocha                  wa Mpira wa Miguu Tanzania (TAFCA).
        IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA 
        MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
        
Comments
Post a Comment