MACHESTER UNITED YAKARIBIA KUMNASA KIPA VICTOR VALDES KWA USAJILI HURU …nyota huyo wa zamani Barcelona tayari aanza kujifua United


MACHESTER UNITED YAKARIBIA KUMNASA KIPA VICTOR VALDES KWA USAJILI HURU …nyota huyo wa zamani Barcelona tayari aanza kujifua United

KIPA wa zamani wa Barcelona Victor Valdes amefanya mazoezi na kikosi cha kwanza cha Manchester United Ijumaa kwenye ngome yao ya Carrington na anategemewa kukamilisha usajili wa kuduwaza Old Trafford wiki mbili zijazo.

Victor Valdes ambaye ni mchezaji huru, yuko kwenye maongezi na kocha wa United Louis van Gaal.

Wakala wa Valdes, Gines Carvajal pamoja na wawakilishi wake wengine, wamekutana uongozi wa United huku Van Gaal akiwa na kiu ya kukamilisha usajili huo ndani ya siku chache zijazo.

Kwa muda mrefu Valdes alikuwa akihusishwa na safari ya kwenda Liverpool, lakini sasa mchezo umegeuka United ikionekana kupiga hatua kubwa zaidi.



Comments