Licha ya kufunga bao lililoinusuru timu yake kupokea kichapo kutoka kwa wageni Chelsea katika mchezo wa jana, kocha Luis Van Gaal wa Manchester United alichukizwa na ushangiliaji wa mshambulizi, Robbin Van Persie mara baada ya kufunga bao la kusawazisha katika dakika ya mwisho ya mchezo.
" Kilikuwa ni kitendo cha kipuuzi, naona alikuwa na furaha ila          alipewa kadi ya njano. Huo si uelevu sana' alisema Van Gaal          alipokuwa akizungumzia kitendo cha mshambulizi wake kushangilia          na kuvua jezi mara baada ya kufunga.
          
          Baada ya kumalizika kwa mchezo huo uliopigwa katika dimba la Old          Trafford, Van Gaal aliweka wazi kutofurahishwa na ushangiliaji          wa nahodha huyo wa United ambaye alivua jezi yake. Kocha huyo          raia wa Uholanzi ambaye timu yake itacheza na mahasimu wao wa          jiji la Manchester mwishoni mwa wiki hii aliisifu timu yake kwa          namna ilivyocheza.
" Chelsea walijaribu kuimaliza mechi mapema. Waliufanya uwanja uwe mkubwa hivyo tulilazimika kukimbia sana uwanjani. Tulipigana hadi mwisho. Tulistahili kufunga bao la kusawazisha, tulitengeneza nafasi nyingi zaidi ya Chelsea."
Kikosi cha Jose Mourinho hakikutengeneza nafasi nyingi za kufunga katika mchezo huo ambao unawafanya kumaliza msimu wa tatu mfululizo pasipo kupoteza mbele ya United katika mchezo huo; ' Chelsea walitengeneza nafasi moja katika kipindi cha kwanza, mawasilliano yetu yalipotea na kutoa nafasi kwao kufunga bao. Bao lile lilituchanganya lakini tuliendelea kucheza vizuri sana.
Comments
Post a Comment