LOUIS VAN GAAL AMFAGILIA KINOMA JOSE MOURINHO


LOUIS VAN GAAL AMFAGILIA KINOMA JOSE MOURINHO

Manchester United manager Louis van Gaal has played                  down his role in Jose Mourinho's success as a boss

LOUIS van Gaala ametupilia mbali hisia zilizojengeka miongoni mwa wadau wa soka kwamba yeye ndiye aliyemtengeneza Jose Mourinho kuwa Special One.

Van Gaal insists Chelsea manager Mourinho                  (pictured) became the Special One all by himself

Kocha huyo wa Manchester United amesisitiza kuwa Mourinho amejitengeneza mwenyewe kuwa Special One.

Van Gaal anakumbana na mtihani mkubwa zaidi tangu aanze kuikochi Manchester United Jumapili hii wakati atakapokumbana na Chelsea ambayo bado haijapoteza mchezo hata mmoja.

Mechi hiyo itakayopigwa Old Trafford, itatoa picha halisi kama Manchester United ni mshindani wa kweli kwenye kusaka taji au  ni msindikizaji.

Van Gaal alifanya kazi na Jose Mourinho miaka 17 iliyopita wakati alipomjumuisha Mreno huyo akiwa na umri wa miaka 34 kwenye safu yake ya makocha Barcelona na kuanzia hapo imekuwa ikiaminika kuwa Van Gaal ndiye aliyemjenga Mourinho kuwa hivyo alivyo. 



Comments