KIPA SIMON MIGNOLET KIKAANGONI ANFIELD …LIVERPOOL YATEGA NDOANO KWA KIKO CASSILLA WA ESPANYOL




KIPA SIMON MIGNOLET KIKAANGONI ANFIELD …LIVERPOOL YATEGA NDOANO KWA KIKO CASSILLA WA ESPANYOL

Options: Espanyol's Kiko Casilla is also on                    Arsene Wenger's list of targets

LIVERPOOL imempa ofa kipa wa Espanyol, Kiko Casilla (pichani) kujiunga na klabu yao katika usajili wa Januari kuwa mbadala wa Simon Mignolet.

Casilla amekuwa akifuatiliwa kwa kiana na wasaka vipaji wa Reds msimu huu, wakati timu hiyo ikiwa katika msako wa kipa mwingine – na Brendan Rodgers sasa ameamua kumfanyia kweli.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Hispania, Liverpool wamepeleka pendekezo kwa Casilla wakimtaka kutua Anfield mwaka mpya na kuwa chaguo lao namba moja langoni.

Habari za ndani zinaeleza kuna klabu nyingine kadhaa zimepeleka maombi kwa Casilla ikiwamo Real Madrid, lakini Liverpool ina ujasiri wa kufanya biashara na kipa huyo.



Comments