KATIBU MKUU SIMBA SC; ‘TUTAMFUKUZA KAZI PATRICK PHIRI’



KATIBU MKUU SIMBA SC; 'TUTAMFUKUZA KAZI PATRICK PHIRI'

Na Baraka Mbolembole

bb

( Makamu wa rais wa klabu ya Simba SC, Geofrey Nyange Kaburu ( anayetazama Kamera) akifuatilia moja ya michezo ya timu yake)
Uongozi wa klabu ya soka ya Simba SC umetangaza kumpatia mechi mbili kocha wao Mzambia, Patrick Phiri . Simba imekuwa na mwanzo mgumu msimu huu katika ligi kuu Tanzania Bara baada ya kutoa sare tano mfululizo katika michezo mitano iliyokwisha chezwa hadi sasa. Ikiwa nyuma ya vinara Mtibwa Sugar kwa tofauti ya point inane, Simba imepitwa pia na timu za Azam FC na Yanga kwa tofauti ya pointi tano.

Simba itacheza mchezo wa pili msimu huu katika uwanja wa ugenini wakati watakapoikabili Mtibwa, mchezo wa raundi ya saba utakuwa ni ule dhidi ya Ruvu Shooting ya Pwani katika uwanja wa Taifa, kama timu itakosa matokeo katika michezo hiyo kocha huyo aliyepokea kazi ya Mcroatia, Zdravko Logarusic mapema mwezi Agosti akitokea timu ya Green Buffaloes ya ligi ya Zambia.

Mchezo wa Jumamosi hii dhidi ya Mtibwa katika uwanja wa Jamhuri unaweza kumuondoa kocha huyo ndani ya miezi miwili kama atashindwa kuisaidia timu yake kupata ushindi. Kipigo kitavunja mahusiano ya kikazi kati ya klabu na mwalimu huyo ambaye aliomba ruhusa ya kwenda kwao mara baada ya sare dhidi ya Tanzania Prisons wiki iliyopita katika uwanja wa Sokoine, Mbeya.
bb2

( Hiki ndiyo kikosi ndicho kinatajwa kuwa bora zaidi katika klabu ya Simba tangu kizazi cha mwaka 1993. Chini ya kocha Mkenya James Siang'a, Simba ilifanikiwa kufika hatua ya robo fainali ya klabu bingwa Afrika, ' Ligi ya Mabingwa Afrika', 2003. Evance Aveva rais wa sasa wa timu hiyo alikuwa mmoja wa watu waliofanikisha usajili wa wachezaji, Juma Kaseja, Athumani Machuppa, Ulimboka Mwakingwe, Victor Costa, Christopher Alex ambao katika msimu wao wa kwanza tu walifanya mambo makubwa.)

Uongozi ulimnyima ruhusa ya kwenda kwao wakati huu timu ikiwa imrweka kambi ya muda mfupi Mkoani, Iringa kujiandaa na mchezo wa Jumamosi hii. UOngozi wa klabu hiyo umefikia hatua ya kumpatia mechi mechi mZambia huyo baada ya kushindwa kupata ushindi wowote. Phiri ameambiwa ni lazima abadili mwendo wa ' sare, sare' kama anataka kuendelea kufanya kszi yake katika timu hiyo.

Akizungumza na vyombo vya habari, Katibu mkuu wa klabu hiyo Steven Ally alisema Phiri anatakiwa kubadili mwenendo wa matokeo mabaya katika timu na michezo dhidi ya Mtibwa na Shooting itamuweka ' kikaangoni' kama timu haitashinda

." Kilichotokea ni kwamba, siku ya tarehe 27, 2014 katika kikao cha kamati ya ufundi pamoja na uongozi wa Simba Sports Club, kikubwa tulijadili kuhusu muendelezo wa ligi kuu ya Vodacom pamoja na kiwango cha timu kiujumla kutokana na matokeo tuliokuwa tukiyapata. Matokeo ya droo mfululizo, kamati ya ufundi ilikutana pamoja na benchi la ufundi wakiwa na nia ya kuangalia mustakabali na tatizo linatokea wapi. Makubaliano ' kadha wa kadha' yalifikiwa kutokana na kikao hicho cha 27 Oktoba, 2014. Miongozo minne ilitolewa kama ifuatavyo"

" Kwanza; Kutokana na maandalizi makubwa yaliyopangwa na mchakati mzima wa kuanza ligi hadi tulipofikia sasa, ilionekana kwamba benchi la ufundi lipewe mechi mbili za kuweza kurekebisha matokeo na kiwango cha timu kwa ujumla. Baada ya mechi hizo kumalizika kutakuwa na kikao cha kutathimini mechi hizo na zile zote zilizotangulia ili kuona mbele tutakwenda kufanya nini."
hans

( Zacharia Hans Poppe, Mwenyekiti wa kamati ya usajili ya Simba SC)

Zacharia Hans Poppe kwa upande wake anasema kuwa wanaeendelea kufanya utafiti ili kubaini kama kweli kocha wao hana uwezo wa kuinoa timu hiyo, na endapo watajidhihirisha ni , Ndiyo, watamuondoa; " Kama tatizo litakuja kujulikana si wachezaji basi mwalimu atawajibika. Kocha mwenyewe mbinu zake ndizo zimepelekea mambo kuwa hivyo hakuna namna ataondolewa kwa kuwa lengo letu ni kujenga timu" alinukuliwa akisema Mwenyekiti huyo wa kamati ya usajili.



Comments