Leo                      ndo siku ambayo aliyekua msanii wa kundi la Wanaume                      Family 'YP' amezikwa ikiwa imepita siku moja tu                      tangu afariki dunia. Chanzo cha kifo cha msanii huyo                      ni ugonjwa wa kifua ambao ulikua ukimsumbua kwa mda                      mrefu. Bongoclan imepata nafasi ya kufanya mahojiano                      na Juma Nature ambapo alisema ni huzuni kubwa sana                      kumpoteza msanii mwenzake ambaye walikua wakifanya                      kazi pamoja tangu zamani.
                                      Pia                              tuliweza kumuuliza ni kitu gani anajivunia                              kuhusu mziki wake na alikua na haya ya                              kusema " Mimi najivunia nina mashabiki wengi                              kuliko mtu yeyote Tanzania, nina mashabiki                              wengi sana ambao hawana fitna na sio wa                              kutengenezwa. Wanaotengeneza mashabiki huo                              ni ulimbukeni kwa sababu labda ni tamaaa za                              pesa, kuna mtu mwingine anataka kutengeneza                              kitu labda anataka kua mtu flani kwa                              kuforce. Mziki tuliokua tunafanya sisi sio                              wa kutengeneza kama mtu anaomba nyimbo yako                              redion anaomba sio kwamba msanii kamwambia                              piga simu uombe nyimbo yangu redion. Sasa                              athari zake tutakosa msanii bora ambaye                              ataiwakilisha Tanzania au hata Afrka.
                                            Habari                              imeandikwa na Eddie Sucre na Sweetbert                              Abednego wa Zenji Fm
                      
Comments
Post a Comment