HATIMAYE MARIO BALOTELLI AZISABAHI NYAVU LIVERPOOL IKIINYUKA SWANSEA 2-1 CAPITAL ONE CUP


HATIMAYE MARIO BALOTELLI AZISABAHI NYAVU LIVERPOOL IKIINYUKA SWANSEA 2-1 CAPITAL ONE CUP

Coutinho congratulates Balotelli after he scores                  only his second goal since his summer move from AC                  Milan

HATIMAYE Mario Balotelli amevunja ukimya wake wa kuzifumania nyavu baada ya kuifungia Liverpool kwenye mchezo mkali wa Capital One Cup ulioshuhudia wekundu hao wakiibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Swansea.

Hata hivyo ushindi wa Liverpool haukuja kirahisi kwani walitanguliwa kwa bao la dakika ya 66 kupitia kwa Marvin Emnes na ikabidi wasubiri hadi dakika ya 86 pale Balotelli aliposawazisha akiunganisha vizuri krosi ya Fabio Borini.

The Italian firebrand equalises for Liverpool                  within seconds of his introduction with a volley between                  two Swansea defenders

Wakati ikionekana mpira utamalizika kwa sare ya 1-1, Federico Fernandez  akalambwa kadi nyekundu kwa kumchezea rafu mshambuliaji Philippe Coutinho katika dakika za nyongeza (za majeruhi) kisha ukapigwa mpira wa free-kick uliounganishwa wavuni kwa kichwa na beki Dejan Lovren – Liverpool wakaibuka washindi.

Liverpool: Jones, Manquillo, Toure, Lovren, Johnson, Lucas, Henderson, Markovic (Lallana 70), Coutinho, Borini, Lambert (Balotelli)

Swansea: Tremmel, Rangel, Fernandez, Williams, Taylor, Dyer (Routledge 67'), Fulton (Carroll), Shelvey, Montero, Gomis (Bony), Emnes. 



Comments