Jackson Issa Nundu mwanamuziki ambaye siku zote alijulikaa kwa jina la Iss Nundu amezikwa leo mchan Moshi mjini. Issa Nundu alifariki Jumamosi alfajiri katika hospitali ya KCMC alikokuwa amelazwa baada ya kuhamishwa kutoka Kigoma.
Wanamuziki waliwakilishwa na wanamuziki wawili wakongwe mpiga saxophone Yusuph Bernard na Mmwanamuziki mwingine Mohamed Mwinyjuma(Baba yak e Mwana FA).Ibada ya mazishi ilifanyika katika kanisa la Kristu Mfalme na kuongozwa na Padri Sosthenes Bahati. Wanamuziki wa Dar es Salaam walichangia rambirambi zao kupitia kwa Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanamuziki John Kitime, katika michango hiyo Mheshimiwa January Makamba pia alitoa mchango mkubwa, fedha hizo zilianza kusaidia ktika kulipia ghrama za hospital na pia kusaidia kuwasafirisha wazazi wa marehemu kurudi kwao Kongo. Fedha hizo zilikabidhiwa kwa familia kupitia kwa mwanamuziki Mohamed Mwinyijuma…picha za matukio
ISSA NUNDU ALIZALIWA 23/7/1954 NA KUFARIKI 25/10/2014
Padri Sosthenes Bahati akimuombea marehemu kabla ya kupelekwa makaburini
KUSHOTO GREYSON KAKIGWA MPENZI WA MUZIKI HASA WA ZAMANI AMBAYE ALISOMA HISTORIA FUPI YA MAREHEMU KWA NIABA YA FAMILIA
Comments
Post a Comment