
Mwezi, Wiki na Siku zikabaki, Masaa                   kwa ile Filamu Mpya na ya Kusisimua ya MAPENZI YA                  MUNGU Kuingia Sokoni, Sasa filamu hiyo yaingia sokoni                  leo ambayo imewakutanisha wasanii mahiri wa hapa hapa                  Tanzania ambapo Mmoja kati ya Wasanii waliocheza filamu                  hiyo Ni Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya anayejulikana                  kama Linah Sanga, kwa Kushirikiana na Elizabeth Michael                  bila Kumsahau                  Flora Mtegoha ambae ni Mama Mzazi wa Marehemu Steven                  Kanumba watakuwa ndani ya filamu Mpya iitwayo MAPENZI YA                  MUNGU...Ni Filamu ambayo Kisa chake na Mafunzo yake                  yanasisimua lakini Pia ni Moja kati ya filamu ambayo                  kiukweli ina hadhi na vigezo vya kimataifa......
              
Nimefika hapa leo sio kwa Ujanja wangu Bali ni Kwa "Mapenzi ya Mungu..."
            
          Nimefika hapa leo sio kwa Ujanja wangu Bali ni Kwa "Mapenzi ya Mungu..."
Filamu ya "Mapenzi ya Mungu" ni                  moja ya filamu ambayo Msanii Linah pamoja na Mama Mzazi                  wa Marehemu Kanumba wameonyesha uwezo wa hali ya juu na                  kuthibitisha kuwa kweli Sanaa ni Kazi.
          Filamu ya "Mapenzi ya                  Mungu" itakuwa Sokoni Kuanzi Wiki hii Kwa Wauzaji wa                  Filamu kote Nchini.
          Filamu hii itasambazwa na                  Kampuni mahiri ya Proin Promotions Ltd.
        
Comments
Post a Comment