FIFA yataja 23 wanaowania Ballon d’Or 2014.



FIFA yataja 23 wanaowania Ballon d'Or 2014.

Shirikisho la soka duniani FIFA limetangaza majina ya wachezaji 23 wanawania tuzo ya FIFA Ballon d'Or mwaka 2014.
Timu ya taifa ya Ujerumani imetoa wachezaji sita katika kinyang'anyiro cha tuzo hizo, nyota hao ni Philipp Lahm, Mario Gotze, Toni Kroos, Thomas Muller, Manuel Neuer na Bastian Schweinsteiger.
Timu za Real Madrid pamoja Bayern Munich zimetoa wachezaji sita wanaowania tuzo hiyo, wachezaji wanne wa Barcelona watatu wa Chelsea, wakati Manchester United, Manchester City, Paris Saint-Germain, Juventus zote zimetoa mchezaji mmoja mmoja kwenye tuzo hiyo.

12
Wachezaji wanao wania tuzo hiyo ni pamoja na Gareth Bale (Wales), Karim Benzema (France), Diego Costa (Spain), Thibaut Courtois (Belgium), Cristiano Ronaldo (Portugal), Angel Di Maria (Argentina), Mario Gotze (Germany), Eden Hazard (Belgium), Zlatan Ibrahimovic (Sweden), Andres Iniesta (Spain), Toni Kroos (Germany), Philipp Lahm (Germany), Javier Mascherano (Argentina), Lionel Messi (Argentina), Thomas Muller (Germany), Manuel Neuer (Germany), Neymar (Brazil), Paul Pogba (France), Sergio Ramos (Spain), Arjen Robben (Netherlands), James Rodriguez (Colombia), Bastian Schweinsteiger (Germany), Yaya Toure (Ivory Coast)
katika majina hayo 23 hakuna jina la mshambuliaji Luis Suarez japo aliisaidia Liverpool kwa kufunga magoli ya kutosha msimu uliopita.



Comments