EL CLASICO: MADRID IKIMKOSA BALE – BARCA WANA SUAREZ


EL CLASICO: MADRID IKIMKOSA BALE – BARCA WANA SUAREZ

Na Baraka Mbolembole,

Leo Messi alifunga ' Hat-trick' katika mchezo wa mwisho wa mahasimu wa soka la Hispania. El Clasico ni mechi kubwa zaidi ya soka nchini Hispania ambayo inafuatiliwa na wapenzi wengi wa soka barani Ulaya, Real Madrid na FC Barcelona ndiyo timu zinazotengeneza mechi hiyo ambayo itachezwa kwa mara nyingine siku ya kesho Jumamosi katika uwanja wa Santiago Bernabeu.

Machi mwaka huu timu hizo zilikutana mara mbili katika uwanja wa Bernabeu. Mara ya kwanza ilikuwa ni katika mchezo wa La Liga na Barcelona ilishinda kwa mabao 4-3 huku akifunga mabao matatu kwa mpigo ' hat-trick'. ' Los Blancos' walishinda kwa mabao 2-1 na kutwaa ubingwa wa Copa Del Rey. Gareth Bale alifunga ' moja ya mabao yenye thamani kubwa' katika mchezo huo. Bale alikimbia kwa kasi, akamzunguka mlinzi wa Barcelona Marco Barta na kwenda kufunga bao la ushindi kwa timu yake zikiwa zimesalia dakika saba mchezo umalizike.

Katika ' sura na ubora' tofauti, timu hizo zitapambana katika mchezo wa raundi ya nane msimu huu. Barcelona haijaruhusu bao lolote katika ligi ya La Liga . Barca itakwenda Santiago ikiwa na hali kubwa, wameshinda mara saba katika michezo nane msimu huu chini ya kocha Luis Enlique ambaye huo utakuwa mchezo wake wa kwanza wa ' Clasico' kushiriki kama kocha.

' Blaugrana' wamefunga mabao 22 katika michezo nane iliyopita lakini watakuwa na wakati mgumu kuithibiti timu kali katika mashambulizi. Los Blancos walianza msimu kwa kiwango cha chini, lakini mambo yanakwenda sawa tangu walipoishinda Derpotivo la Coruna kwa mabao 7-2 katika uwanja wa Riazor, mwezi uliopita. Kiungo na kaimu nahodha wa Barca, Andres Iniesta tayari amesema kuwa mechi hiyo ni zaidi ya ' kusaka pointi tatu'.

Gareth-Bale-v-Barcelona-October-2013_3104720

Real Madrid watakosa huduma ya Bale, wakati upande wa pili watakuwa wakimkaribisha kikosini kwa mara ya kwanza mshambulizi, Luis Suarez ambaye alifungiwa na Shirikisho la soka duniani, FIFA tangu mwezi Juni kutokana na kumng'ata meno mlinzi, Giorgio Chiellini wa Italia wakati wa mchezo wa kombe la dunia kati ya Uruguay na Italia, nchini Brazil. Suarez ambaye aliruhusiwa kucheza ' michezo isiyo rasmi' mwezi huu wakati Uruguay ilipokuwa barani Asia kucheza na Saud Arabia na Oman ataonekana kwa mara ya kwanza katika kikosi cha Barcelona.

 

Hii inaweza kuwa mechi ngumu kwa wenyeji ambao watakabiliana na ' wachezaji bora kutoka Amerika Kusini' katika safu ya mashambulizi. Neymar tayari amefunga mara mbili katika michezo mitatu ya ' Clasico' huku Messi akiwa anaongoza chati ya mfungaji bora wa muda wote katika ' Clasico'. Real Madrid ilifunga mabao matatu katika muda wa dakika 41 katika uwanja wa Anfield katikati ya wiki hii walipoishinda Liverpool kwa mabao 3-0 katika ligi ya mabingwa, iatakuwa na wachezaji wake watatu waliofanya mambo makubwa siku ya Jumatano.

 

Karim Benzema alifunga mara mbili, wakati Cristiano Ronaldo alifunga mara moja baada ya ' kupokea pasi bab-kubwa' kutoka kwa kiungo, Mcombia, James Rodriguez. Kukosekana kwa Bale inaweza kuwa tatizo kubwa hasa kama wachezaji Andres Inesta, Ivan Rakitic na Sergio Busquets watatawala eneo la katikati ya uwanja. Bale alikuwa na nguvu ya ziada, ana uwezo wa kufuata mipira nyuma na kupita nayo kwa kasi katikati ya uwanja. Real wataingia katika ' Clasico' wakiwa bila Bale na Angel Di Maria ambaye kwa sasa yupo Manchester United ya England.

 

Licha ya kiwango chake kuwa juu, kiungo, Mcroatia, Rakitic atakuwa na sababu zote za kumzima Luka Modric mchezaji mwenzake katika timu ya Taifa. Chachu ya ushindi wa Real Madrid dhidi ya Barcelona katika baadhi ya michezo ni uwezo wa Modric, vurugu za mlinzi, Pepe na uchezaji wa ' ki-Madrid wa Sergio Ramos, mambo yalipokuwa magumu mbinu za kukimbiza mipira zilifanya kazi,na hapo ndipo umuhimu wa wachezaji kama Bale unapohitajika.

 

Ramos hakucheza wala hakuwa katika benchi wakati wa mchezo uliopita dhidi ya Liverpool, Marcelo atakuwa na jukumu zito, mchezaji mmoja kati ya Neymar au Suarez atakuwa akikimbia na mipira katika upande wake, pia anaweza kukutana na usumbufu wa Pedro Rodriguez mchezaji mwingine wa hatari katika Clasico.

 

Real ni kali katika mashambulizi lakini wana matatizo katika ngome. Real Sociedad walifunga mabao manne mwezi uliopita walipotoka nyuma ya mabaso 2-0 na kushinda dhidi ya vigogo hao kwa mabao 4-2 baada ya kumalizika kwa dakika 90. Barca ni timu kali zaidi katika mashambulizi, hata kabla ya Suarez mambo yamreoneka kuwa safi kwa Enlique. Gerlad Pique anaweza kucheza na Javier Mascherano ama Batra katika nafasi za ulinzi wa kati. Dan Alves na Jord Alba watacheza sehemu za pembeni na safu hiyo ya ulinzi imekuwa bora sana tangu kuanza kwa msimu.

 

Nani mshindi katika mchezo huu? Kete yangu naiweka kwa Barca kwa sababu wanaweza kufunga mabao matatu hadi zaidi katika mchezo huo ukilinganisha na Real Madrid. Real wanaweza kufunga bao moja, pengine wakajitahidi na kufunga mabao mawili lakini watalazimika kusahau kila kitu walichofanya msimu huu na kuwa tayari kwa mapambano.

 

MATOKEO YA AINA YAKE AMBAYO BARCA WAMEWAHI KUYAPA, Santiago Bernabeu……..

Johan-Cruyff-1974

1973/14; Johan Cruyff ' aliichanachana' Bernabeu, Barca ikiishinda Real 5-0

Barcelona ilikuwa katika kipindi kigumu kwa muongo mmoja. Wakati muongo wa pili bila taji la La Liga ulipofika mwaka wan ne, Barca iliondoka katika ' unyonge wa bila mataji'. Ikiwa na kiungo mchezesha timu raia wa Uholanzi, Johan Cruyff aliibadili timu hiyo kutoka ' goi-goi' na kuwaongoza kuibuka na ushindi wa ' maangamizi' kwa mahasimu wao Real Madrid.

Cruyff alichukua pasi akiwa katikati ya uwanja, akaanza kuwalamba chenga walinzi wa Real mmoja baada ya mwingine kisha kumfunga kiurahisi golikipa, MarianonGarcia Remon akiwa katika ' kisanduku cha kupigia penalti'. Barcelona ilikuwa kali sana msimu huo na ilichomoza na ushindi wa mabao 5-0 katika uwanja wa Santiago Bernabeu, huku wakitwaa ubingwa michezo mitano kabla ya kumalizika kwa msimu.

1984/85; ilikuwa ni siku ya waingereza, Gary Liniker, Mark Hughes

article-0-1B974995000005DC-116_964x670Real Madrid ilifungwa mabao 3- katika uwanja wa nyumbani na mahasimu wao Barcelona ambao walikuwa chini ya mwalimu, Muingereza, Terry Venables. Mshambulizi wa zamani wa England, Gary Liniker alifunga mara mbili, huku mshambulizi wa Wales, Mark Hughes akifunga lingine na kuipa ushindi wa 3-0 Barca katika uwanja wa Bernabeu

 

2005/06; Gaucho alipigiwa makofi Santiago Bernabeu, ni ajabu!

Barcelona's Ronaldinho celebrates goal against Real              Madrid during Spanish first division soccer match in Madrid

Akiwa na tuzo ya mchezaji bora wa dunia, 2005, kiungo raia wa Brazil, Ronaldinho Gaucho alikuwa na kila sababu ya kutamba. ' Muuaji mwenye tabasamu' ndiyo jina ambalo mashabiki wengi wa soka walipenda kumuita mchezaji huyo wa ' aina yake ambaye hakudumu katika soka la ulaya. Zinedine Zidane alimpiga ' tobo' Gaucho wakati wawili hao ' wenye radha' walipokutana.

 

Kumpiga tobo mcchezaji wa Brazil ni ' sawa na tusi', Gaucho alimpigia makofi mpinzani wake huyo kisha akaja kumjibu kwa kanzu maridadi iliyoambana na tobo. Hakuishia hapo Gaucho aliwapiga chenga walinzi kadhaa wa Real kisha kufunga bao la pili kwa timu yake baada ya Samuel Eto'o kutangulia kufunga. Wakati mechi ilipomalizika na Real licha ya kulazwa mabao 2-1, mashabiki wa Santiago Bernabeu waliinuka katika viti vyao na kumpigia makofi Gsucho na kikosi cha Barca ambacho kilipiga kandanda la kuvutia. Inasemekana mambo aliyofanyiwa Zidane na Gaucho katika mchezo huo ndiyo yaliyosababisha akastaafu soka la ushindani akiwa na miaka 34.

 

2008/09; Unakumbuka, Real Madrid 2-6 FC Barcelona pale Santiago Bernabeu….

real-madrid-fc-barcelone

Ilikuwa ni siku ya aibu' kwa Real Madrid baada ya kuchakazwa katika uwanja wa nyumbani kwa mabao 6-2. Messi alikuwa katika ubora wake na ni wakati ambao alianza kuaminiwa na dunia kama mchezaji bora duniani. Alifunga mara mbili katika ushindi huo mkubwa zaidi katika mechi za ' Clasico', Pique, Sergio Busquets, Thierry Hennry, Xav Hernandez pia walifunga katika mchezo huo.

 

 



Comments