DORTIMUND ‘ BABA LAO’ KUNDI D, YAICHAPA GALA 4-O, ARSENAL ‘ YACHOMOA NA KUMALIZA MECHI USIKU’


DORTIMUND ' BABA LAO' KUNDI D, YAICHAPA GALA 4-O, ARSENAL ' YACHOMOA NA KUMALIZA MECHI USIKU'

Hakuna timu ambayo imeweza kuisimamisha Borussia Dortimund katika kundi D hadi kumalizika kwa michezo ya raundi ya tatu. Dortimund iliifunga Arsenal kwa mabao 2-0 katika uwanja wa Iduna Park Arena, kisha wakashinda mabao 2-1 ugenini dhidi ya Anderlecht, kabla ya jana kuisambaratisha Galatasaray ikicheza pia ugenini.

Pointi tisa katika michezo mitatu huku wakirejea kucheza uwanja wa nyumbani wiki mbili zijazo, Dortimund imekuwa timu kali katika kundi hilo ambalo awali lilionekana kuwa gumu kwa mtazamo wa kimpira. Akicheza kwa mara ya kwanza michuano ya mabingwa Ulaya , mshambulizi raia wa Gabon, Pierre-Emerick Aubameyang alifunga bao lake la pili katika mchezo wa tatu wa michuano hiyo katika dakika ya sita.

1414010557832_wps_36_Marco_Reus_of_Borussia_Do

Galatasaray ambao walikuwa na wachezaji kadhaa wenye majina makubwa kama vile Filepe ,Melo, Wesley Sneijder, Hamit Altintop, Burak Yilmaz na Goran Pandev ilikuwa dhsifu mno. ' Neymar wa Gabon' akafunga bao lake la pili katika mchezo huo huku likiwa bao lake la tatu katika michuano katika dakika ya 18.

Kiungo ambaye alikuwa nje ya uwanja kutoka na majeraha katika miezi ya karibuni, Marco Reus alifunga bao la tatu kwa timu yake na kufanya hadi mapumziko, wenyeji kuwa nyuma kwa mabao 3-0. Zikiwa zimesalia dakika saba mchezo kumalizika, kiungo Adrian Ramos alifunga bao la nne kwa timu yake. Ramos kiungo raia wa Colombia alifunga bao hilo dakika moja baada ya kuingia uwanjani kuchukua nafasi ya Shinji Kagawa katika dakika ya 82.

' Hakuna kukata tama katika mchezo wa soka'. Arsenal ' ilisafa' ;akini mwisho wa mechi walipumzika vizuri baada ya ushindi ' usiotarajiwa' dhidi ya wenyeji Anderlecht ambao walitawala mchezo kwa dakika 70. Wenyeji walishambulia sana huku wakipiga mashuti 14, target yao mbovu ilifanya wajutie mwisho wa mchezo baada ya ' kunyang'anywa' ushindi waliotakiwa kuupata. Anderlecht walipiga mashuti matatu tu ya hatari katika lango la Damian Martinez golikipa huyo mwenye miaka 22 ambaye alipangwa kwa mara ya kwanza na kocha, Arsene Wenger.

Martinez aliweza kuokoa mabao manne ya wazi ambayo wenyeji walikaribia kufunga, licha ya kiungo kinda, Andy Najar, 21 kuwafungia wenyeji bao la kuongoza katika dakika ya 71. Joel Campbell aliingia kuchukua nafasi ya Danny Welbeck dakika nne baada ya Arsenal kufungwa bao, Alex Oxlade Chamberlain pia aliingia kuchukua nafasi ya kiungo mkabaji Mathieu Flamini. Yalikuwa ni mabadiliko mawili ya ' mpigo' na Arsenal ilianza kucheza mchezo wa kushambulia, lakini bado mambo yalikuwa magumu.

1414010703204_Image_galleryImage_Arsenal_s_Polish_born_Ger

Golikipa, Slivio Proto alikuwa imara katika lango lake . Wenger akampumzisha kiungo Jack Wilshere na kumuingiza uwanjani ' mchezaji asiye na furaha' mshambulizi, Lukas Podolski katika dakika ya 84. Aaron Ramsey, Santi Cazorla, Alexs Sanchezi na Chamberlain walianza kukimbia na mipira huku wakihakikisha hawaipotezi kwa urahisi. Muda ulikuwa unayoyoma na ilionekana kama Arsenal wangepoteza mechi.

Mlinzi wa kushoto, Kieran Gibbs aliifungia timu yake bao la kusawazisha katika dakika ya 89. Kisha, Podolski akafunga bao la ushindi katika dakika ya mwisho na kuifanya Arsena kuwa na pointi sita katika nafasi ya pili. Pointi tano zaidi ya timu za Anderlecht na Galatasa



Comments