BARCELONA CHA MTOTO KWA REAL MADRID …YAPIGWA 3-1 KAMA KUMSUKUMA MLEVI …Ronaldo 1 - Messi 0



BARCELONA CHA MTOTO KWA REAL MADRID …YAPIGWA 3-1 KAMA KUMSUKUMA MLEVI …Ronaldo 1 - Messi 0

Luis Suarez is tackled during a frustrating El                  Clasico for Barcelona's new striker as Real Madrid win                  at the Bernabeu on Saturday evening

REAL Madrid wamechanua kwenye La Liga baada ya kuwachapa watani wao wa jadi Barcelona 3-1 na kuzidi kupunguza pengo baina yao ambapo sasa wanatenganishwa na pointi moja tu.

Neymar aliwanyamazisha wenyeji kwa bao la dakika 3 baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Luis Suarez ambaye alikuwa anaichezea kwa mara kwanza Barcelona tangu afungiwe kwa kosa la kumng'ata mchezaji kwenye World Cup.

Lakini Ronaldo alirejesha utulivu dakika ya 35 pale alipoisawazishia Real Madrid kwa penalti.

Beki wa kati wa Real Madrid, Pepe akafunga bao la pili dakika 50 kabla ya Karim Benzema kufunga kitabu cha magoli dakika ya 61.

Supastaa wa Barcelona Lionel Messi alishindwa kuisadia timu yake huku mpinzani wake mkubwa Cristiano Ronaldo akiendelea kuwa mtambo wa magoli.

Lionel Messi (right) looks frustrated during the El                  Clasico match as Real Madrid's Ronaldo (left) beat his                  Barcelona opponent on Saturday

 

Real Madrid were welcomed to the match by a huge                crowd of fans outside the Bernabeu ahead of their win over                rivals Barcelona

 

Angalia umati wa mashabiki waliokuwa nje ya uwanja kuilaki Real Madrid ikiwasili kuikabili Barcelona



Comments