BAADA YA KUSIMAMISHWA MASHUJAA BAND, JADO FFU AJIPOZA NA SHOW YA MALAIKA BAND ...akutana na George Gama
MWIMBAJI wa Mashujaa Band aliyesimamishwa kwa wiki mbili Jado FFU, Alhamisi iliyopita aliamua kujivinjari kwenye onyesho la Malaika Band.
Kama anavyoonekana pichani, Jado akajitosa kwenye ukumbi wa Kituro Night Club ulioko Mabibo na kuwa mmoja wa watazamaji wa onyesho hilo la Malaika ambalo lilifana sana.
Katika onyesho hilo, Jado akapata wasaa pia wa kukutana na mpiga bass maarufu George Gama (pichani chini) ambaye bado anasumbuliwa na ugonjwa kwa kupooza.
Comments
Post a Comment