ATLETICO MADRID YASHINDA 5-0, JUVENTUS IKICHAPWA KUNDI A



ATLETICO MADRID YASHINDA 5-0, JUVENTUS IKICHAPWA KUNDI A

Makamu-bingwa wa ulaya, Atletico Madrid wameitandika, Malmo FF ya Sweden kwa mabao 5-0. Hadi kipindi cha kwanza kilipomalizika, Atletico walikuwa wamebanwa. Dakika ya tatu baada ya kuanza kwa kipindi cha pili, kiungo Koke alifungua akaunti ya mabao , mshambulizi, Mario Mandzukic alifunga bao la pili katika dakika ya 61, dakika mbili baadae, mshambulizi, Mfaransa, Gtezmann akafunga bao la tatu.

1414014506610_wps_38_epa04458540_Atletico_Madr

Diego Godin na na Cerci walihitimisha ' kalamu' ya mabao katika dakika tatu za mwisho na kutengeneza ushindi mkubwa zaidi zaidi usiku wa jana katika michuano hiyo. Kwa matokeo hayo, Atletico wamepanda hadi katika nafasi ya pili nyuma ya vinara, Olympiacos ya Ugiriki ambayo iliwalaza mabingwa wa Italia, Juvuntus kwa bao 1-0.

Ikicheza katika uwanja wake wa nyumbani, Karaiskaki, jijini, Athens kiungo raia wa Macedonia, Pajtim Kasami, 22 aliwafungia wenyeji bao pekee katika dakika ya 36 na kufanya timu hiyo kushinda michezo yote waliyocheza nyumbani. Olympiacos waliifunga Atletico Madrid kwa mabao 3-2 katika uwanja huo ilikuwa imara muda wote wa mchezo kiasi cha kuwabana vijana wa kocha Masimilliano Arlegi. Wagiriki hao wanaomgoza kundi la kwanza wakiwa na pointi sita sawa na mabingwa wa Hispania, huku Juventus na Malmo wakishika nafasi za tatu na ile ya nne wakiwa na pointi tatu kila timu.



Comments