ARSENAL KUBISHA HODI BARCELONA USAJILI WA JANUARI …yataka saini ya Pedro


ARSENAL KUBISHA HODI BARCELONA USAJILI WA JANUARI …yataka saini ya Pedro

Overhaul: The 26-year-old could be moved on from                  Camp Nou by new manager Luis Enrique

ARSENAL ipo tayari kuanzisha mazungumzo na Barcelona kuhusu dili la pauni milioni 25 la kumtwaa winga inayemuhitaji, Pedro katika usajili ujao wa Januari.

Pedro, ambaye aliripotiwa kukaribia kutua the Gunners kiangazi kilichopita, ameomba kuondoka Barca katika kipindi cha mwaka mpya baada ya kushindwa maisha ya Camp Nou chini ya kocha Luis Enrique.

Mtandao wa habari wa Fichajes wa Hispania unasema kuwa Arsene Wenger yu tayari kufika bei ya pauni milioni 25 kwa ajili ya kumpata winga huyo mwenye umri wa miaka 27, na anaamini makubaliano yatafikiwa haraka.

Chelsea na Liverpool pia zinahusishwa na mbio za kumuwania winga huyo, lakini Arsenal inaonekana kuwa karibu zaidi kumaliza biashara.



Comments