ARSENAL KAMA WANGA VILE, WABADILI MCHEZO DAKIKA MBILI ZA MWISHO … Gibbs, Podolski wapeleka kicheko Emirates
ARSENAL wamejiweka katika nafasi nzuri ya kuvuzu 16 bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kushinda kimiujiza ugenini dhidi ya Anderlecht katika mchezo mkali wa kundi D.
Hadi dakika ya 89, Arsenal walikuwa nyuma 1-0 kwa bao la Andy Najar la dakika ya 71, lakini beki wa kushoto Kieran Gibbs akairudisha timu yake mchezoni baada ya kuisawazishia bao, kabla ya Lukas Podolski hajafunga goli la ushindi dakika moja baadae.
Ushindi huo unaifanya Arsenal ijikusanyie pointi sita ikiwa nyuma ya vinara Borrusia Dortmund yenye pointi tisa.
Anderlecht: Proto, Vanden Borre, Mbemba, Deschacht, Acheampong, Tielemans, Defour, Najar, Praet (Dendoncker 88), Conte, Cyriac (Suarez 83).
Arsenal: Martinez, Chambers, Mertesacker, Monreal, Gibbs, Flamini (Oxlade-Chamberlain 74), Sanchez, Ramsey, Wilshere (Podolski 84), Cazorla, Welbeck (Campbell 74).
Comments
Post a Comment