ANGEL DI MARIA YUKO FITI KUIVAA CHELSEA ...Carrick naye yu tayari


ANGEL DI MARIA YUKO FITI KUIVAA CHELSEA ...Carrick naye yu tayari

Angel di Maria, shadowed by Chris Smalling, has                  been declared fit to face Premier League leaders Chelsea                  at Old Trafford on Sunday 

HABARI njema kwa mashabiki wa Manchester United ni kwamba Angel di Maria yuko fiti kuivaa Chelsea Jumapili hii.

Mkali huyo aliyesajiliwa kwa pauni milioni 60 kutoka Real Madrid, aliumia mguu katika mechi ya 2-2 dhidi West Bromwich Albion Jumatatu na ilihofiwa kuwa atakasa mchezo huo mkubwa wa kwanza kwake msimu huu.

The £60million signing was pictured sporting an ice                  pack on a thigh injury picked up in the score draw at                  The Hawthorns 

Alifungwa barafu mguuni baada ya kutolewa dakika ya 76 lakini ameweza kufanya mazoezi siku mbili zilizopita na yuko fiti kuivaa Chelsea.

Naye kiungo Michael Carrick aliyekuwa nje ya dimba kwa miezi mitano, anatarajiwa kucheza katika mchezo huo hii ikiwa ni baada ya kujumuishwa katika orodha ya wachezaji wa akiba Jumatatu iliyopita katika mchezo dhidi ya West Bromwich Albion.

 

 



Comments