ALEX SONG SINDANO YA MOTO KWA MAN CITY IKICHUKUA KIPIGO KWA WEST HAM


ALEX SONG SINDANO YA MOTO KWA MAN CITY IKICHUKUA KIPIGO KWA WEST HAM

Alex Song put in a commanding performance for West                  Ham as they beat City 

KIUNGO wa Barclena anayecheza kwa mkopo West Ham, Alex Song, ametakata vilivyo kwenye dimba la kati na kupelekea timu yake kuidhibiti Manchester City na kuisukumizia kisago cha bao 2-1 kwenye mchezo mkali wa Ligi Kuu ya England.

City ambayo ina utajiri wa wachezaji wa viungo, ilishindwa kabisa kumfunika Song ambaye alitibua nyendo nyingi za maadui na kupelekea timu yake kuwa na utulivu kwenye eneo la ulinzi.

Song plays a 'rabona' pass in the penalty area                  during West Ham's win

West Ham iliandika goli lake la kwanza dakika ya 21 kupitia kwa Morgan Amalfitano bao lililodumu hadi mapumziko na ilipotimu dakika ya 75 Diafra Sakho akatupia la pili kabla ya Silva kuchomoa moja dakika mbili baadae.

West Ham (4-1-2-1-2): Adrian 7; Jenkinson 6.5, Collins 7, Reid 6.5, Cresswell 7.5; Song 8; Noble 7, Amalfitano 7 (Kouyate 67 6); Downing 5.5; Valencia 7 (Cole 76), Sakho 7.5 (Nolan 89)

Manchester City (4-4-2): Hart 7; Zabaleta 5, Kompany 4.5, Mangala 3, Clichy 5 (Kolarov 78); Navas 5, Fernando 5 (Milner 78), Toure 5.5, Silva 7; Aguero 6.5, Dzeko 5 (Jovetic 59 5).



Comments