YAMOTO BAND YAJITANUA … YAMVUTA JOSE MARA WA MAPACHA WATATU




YAMOTO BAND YAJITANUA … YAMVUTA JOSE MARA WA MAPACHA WATATU
YAMOTO BAND YAJITANUA … YAMVUTA JOSE MARA WA MAPACHA            WATATU

REMIX ya kibao 'Niseme Nisiseme' cha Yamoto Band, kinachoonekana kufanya vema hivi sasa, iko mbioni kupakuliwa, safari hii ikiwa imemshirikisha nguli wa uimbaji kutoka Mapacha Watatu, Jose Mara.

Akizungumza na SALUTI5 jijini Dar es Salaam, Meneja wa TMK Wanaume Family inayomiliki Yamoto Band, Said Fella alisema kuwa, remix hiyo iko katika hatua za mwisho, huku akiwaomba mashabiki wakae mkao wa kusubiri uhondo wa burudani ya kibao hicho.

Fella alisema kuwa, wameamua kuandaa remix hiyo ili kuzidi kukonga nyoyo za mashabiki wao kutokana na kubaini kwamba wamekiongezea vionjo kibao hicho kilichobeba ujumbe mzito kwa jamii, juu ya tunavyopaswa kuwamakini na watoto wetu majumbani.



Comments