Angel di Maria alitolewa na Louis van Gaal, United wakiwa 3-3 dhidi ya Leicester
WAKIWA katika vyumba vya kubadilishia nguo, wachezaji nyota wa Manchester United walilaumu vikali kitendo cha Angel di Maria kutolewa katika kipigo cha mabao 5-3 dhidi ya Leicester.
Di Maria, ambaye aliifungia United goli la msimu na kuwafanya waongoze 2-0, alikwenda benchi baada ya kufunga bao la tatu kufanya matokeo yawe 3-3.
Baada ya mechi, moja ya chanzo habari kutoka Uwanja wa The King Power kimesema kilisikia wachezaji wa United wakiwaka kweli wakisema: " 'Why the f*** did we substitute Di Maria?'. Hatujaona haja ya kutafsiri kwasababu za kimaadili.
+13
Di Maria (mstari wa nyuma, katikati) akiwa amekaa benchi na kutazamana United ikipoteza 5-3
+13
Van Gaal alimuingiza Juan Mata (mstari wa nyuma, katikati) kuchukua nafasi ya Di Maria zikiwa zimesalia dakika 15 mpira kumalizika.
Mshambuliaji huyo wa Argentina alikuwa mchezaji nyota katika mechi dhidi ya QPR wiki iliyopita. Lakini kocha aliye katika kiti cha moto, Van Gaal, katika dakika ya 76 alimtoa mchezaji huyo aliyesajiliwa kwa paundi milioni 60 kutokea klabu ya Real Madrid
Leicester kiukweli walipata nafuu baada Di Maria kutoka na nafasi yake kuchukuliwa na Juan Mata na walifunga mabao mawili yaliyowapa ushindi mnono.
Van Gaal alimlaumu waziwazi beki wake wa Kibrazil, Rafael kwa kusababisha penalti katika dakika ya 62.
+13
Di Maria alikuwa katika kiwango cha juu
Comments
Post a Comment