VAN GAAL AMPA MIKOBA KINDA WA MIAKA 19 KWENYE UKUTA WA MANCHESTER UNITED …Rojo nae asogezwa katikati, Luke Shaw apewa shavu la kushoto

KOCHA wa Manchester United Louis Van Gaal amempanga kinda wa miaka 19 Patrick McNair kama beki wa kati kwenye mechi ya Ligi Kuu dhidi ya West Ham.

Hali hiyo imekuja kufuatia majanga ya kuwepo kwa majeruhi wengi wakiwemo Chris Smalling, Jonny Evans na Phil Jones huku kinda mwingine aliyeanza mechi zote Tyler Blackett akitumikia adhabu ya kadi nyekundu.

Patrick McNair raia wa Ireland ya Kaskazini, aliingia Manchester United akiwa na umri wa miaka 16 na akawa mchezaji wa kudumu kwenye kikosi cha chini ya miaka 21. Amekuwa akichuana na kinda mwingine Tom Thorpe kuwania kuwemo kwenye kikosi kinachoanza.

Luke Shaw anaanza kama beki tatu huku Marcos Rojo akisogea katikati. Shaw beki chipukizi wa England, 19 amejiunga na United kwa pauni milioni 30 akitokea Southampton, lakini akashindwa kumvutia Van Gaal mazoezini ikiwa ni pamoja na kusumbuliwa na maumivu.

Hata hivyo Shaw ana uzoefu wa kutosha wa mikikimikiki ya Ligi Kuu akiwa ameshaiechezea Southampton mechi 60.

Vikosi vilivyoanza ni: Manchester United: De Gea, Rafael, McNair, Rojo, Shaw, Blind, Herrera, Di Maria, Rooney, Van Persie, Falcao; Subs: Lindegaard, Thorpe, Pereira, Fletcher, Valencia, Januzaj, Mata

West Ham: Adrian, Reid, Cresswell, Tomkins, Demel, Poyet, Song, Amalfitano, Downing, Sakho, Valencia; Jaaskelainen, Nolan, Zarate, Vaz Te, Jenkinson, Collins, Cole

Comments