VAN GAAL AANZA KUONJA JOTO YA WACHEZAJI WA MANCHESTER UNITED …wamcharukia kwanini alimtoa Di Maria



VAN GAAL AANZA KUONJA JOTO YA WACHEZAJI WA MANCHESTER UNITED …wamcharukia kwanini alimtoa Di Maria

Angel di Maria is substituted by Louis van Gaal                    with Manchester United level at 3-3 against Leicester

NYOTA wa Manchester United wakuja juu kwenye vyumba vya kubadilishia nguo kwenye mechi ya kipigo cha 5-3 kutoka kwa Leicester, wakishutumu kitendo cha kocha Louis van Gaal kumpumzisha Angel di Maria.

Di Maria alipelekwa benchi kunako dakika ya 76 wakati huo matokeo yakiwa 3-3 nafasi yake ikichukuliwa na Juan Mata.

Kwa mujibu wa vyanzo kutoka uwanja wa King Power, nyota wa United walionyesha kukwerwa na maamuzi hayo huku mchezaji mmoja akihoji kwa hasira na kutumia lugha chafu: "Kwanini Di Maria alitolewa?

Mkali huyo wa Argentina alikuwa nyota wa mchezo katika ushindi dhidi ya QPR wiki iliyopita. Lakini kocha aliyekalia kiti cha moto, Louis van Gaal, ambaye ameshinda mechi moja tu ya kimashindano tangu alipochukua timu, akampumzisha mchezaji huyo aliyesajiliwa kwa pauni milioni 60 dakika 14 kabla mchezo kumalizika.

Ilikuwa wazi kuwa Leicester waliimarika baada ya Di Maria kutolewa na kutupia wavuni mabao mawili yaliyowapa ushindi.



Comments