TWANGA WAJA NA LADIES NIGHT NDANI YA MACHINGA COMPLEX KILA JUMATANO

TWANGA WAJA NA LADIES NIGHT NDANI YA MACHINGA COMPLEX KILA JUMATANO
TWANGA WAJA NA LADIES NIGHT NDANI YA MACHINGA COMPLEX            KILA JUMATANO

BENDI ya The African Stars "Twanga Pepeta" sasa inakuja kivingine ambapo kuanzia Jumatano hii na kila Jumatano watakuwa na onyesho maalum lililobatizwa Ladies Night.

Onyesho hilo litakuwa likifanyika katika ukumbi wa Business Lounge ulioko kwenye jengo la Machinga Complex Ilala nyuma ya Uwanja wa Karume.

Katika onyesho hilo, wanawake watakuwa wakipewa zawadi za aina mbali mbali kadri watakavyokidhi vigezo.

Mratibu wa maonyesho hayo, Juma Mbizo amedai mbali na zawadi hizo, wanawake watakaoingia ukumbini kabla ya saa nne usiku, watalipa shilingi 2000 tu.

Comments