Affiliated                to FIFA, CAF and CECAFA
           3rd Floor, PPF Tower, Garden                Avenue / Ohio Street
          P.O.                Box 1574, Dar es Salaam, Tanzania     .   Telefax:  +                255-22-2861815
          E-mail: tanfootball@tff.or.tz    .                 Website: www.tff.or.tz
          Release                No. 151
          TAARIFA                KWA VYOMBO VYA HABARI
          Septemba                25, 2014
           TAIFA                STARS, BENIN KUCHEZA DAR OKTOBA 12
          Timu                ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inashuka uwanjani                Oktoba 12 mwaka huu kuikabili Benin katika mechi ya                kirafiki ya kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa                Miguu (FIFA).Mechi hiyo              itachezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10              kamili jioni. Programu ya Taifa Stars inayodhaminiwa na              Kilimanjaro Premium Lager kwa ajili ya mechi hiyo              itatangazwa baadaye na Kocha Mkuu Mart Nooij.Shirikisho la              Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linaendelea na taratibu              nyingine kwa ajili ya mechi hiyo ikiwemo usafiri wa Benin              kuja nchini, ambapo timu hiyo inatarajiwa kutua Uwanja wa              Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Oktoba 10 mwaka              huu ikiwa na msafara wa watu 28.
           Pambano                la Stars na Benin litatanguliwa na mechi ya kudumisha                upendo kati ya viongozi wa dini ya Kikristo na Kiislamu.
           Wakati                huo huo, kutokana na mechi hiyo ratiba ya Ligi Kuu ya                Vodacom (VPL) inafanyiwa marekebisho madogo, na                marekebisho hayo yatatangazwa kesho (Septemba 26 mwaka                huu).
           RAIS                MALINZI KUFUNGA KOZI YA WANAWAKE
          Rais                wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal                Malinzi anatarajia kufunga mafunzo ya uongozi kwa viongozi                wa vyama vya mpira wa miguu wa wanawake vya mikoa ya                Tanzania Bara.
           Hafla                ya kufunga mafunzo hayo itafanyika kesho (Septemba 26                mwaka huu) saa 5 asubuhi kwenye ofisi za TFF, Uwanja wa                Karume, Dar es Salaam.
           Mafunzo                hayo ya siku tano yalishirikisha viongozi 34 wakiwemo                baadhi ya waandishi wa habari na Meneja wa Twiga Stars, na                yaliendeshwa na Mkufunzi wa Shirikisho la Kimataifa la                Mpira wa Miguu (FIFA), Henry Tandau.
           BONIFACE                WAMBURA
          KNY                KATIBU MKUU
          SHIRIKISHO                LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA.
        
Comments
Post a Comment