Mshambuliaji kutoka nchini Uruguay Luis Suarez, bado ana hamu ya kuwa sehemu ya kikosi cha FC Barcelona ambacho kwa msimu huu kipo chini ya meneja kutoka nchini Hispania Luis Enrique Martínez García.
Suarez, anaetumikia adhabu ya kufungiwa kucheza soka katika michuano ya kiushindani kwa kipindi cha miezi minne, ameonyesha hamu ya kutaka kurejea na kujiunga na wachezaji wengine wa FC Barcelona ambapo itakuwa ni mara yake ya kwanza baada ya kusajiliwa akitokea Liverpool, kufutia juhudi anazo zionyesha katika mazoezi pamoja na michezo ya kujipima nguvu ambayo inakihusisha kikosi cha Barcelona B.
Usiku wa kuamkia hii leo, mshambuliaji huyo alieacha gumzo nchini Brazil baada ya kumng'ata beki wa kati wa timu ya taifa ya Italia na klabu ya Juventus Giorgio Chiellini, alicheza mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya taifa ya Indonesia chini ya umri wa miaka 19 ambapo Barcelona B imeichapa Indonesia kwa mabao 6 kwa sifuri.
Kocha wa Barcelona Luis Enrique amesema alitaka Suarez kucheza mchezo huo ili kuwa katika hali ya hamasa ya kimchezo, kabla ya kurejea uwanjani rasmi mwishoni mwa mwezi oktoba.
Suarez anaruhusiwa kushiriki michezo ya kirafiki pekee, na hatashiriki michuano ya ligi ya nchini Hispania La Lila mpaka tarehe 24 mwezi oktoba ambapo Barcelona itakutana na Real Madrid
Comments
Post a Comment