MJUMBE wa Kamati ya Utendaji Simba SC, Collins Frisch jana alibariki ufunguzi wa Tawi jipya la klabu hiyo, liitwalo 'Simba Platinum Supporters', Temeke Pille, jijini Dar es Salaam.
Katika ufunguzi huo uliohudhuriwa na wanachama wengi zaidi wa Tawi hilo, pia Frisch alizindua ukurasa wa facebook uitwao 'Simba Platinum Supporters na Blogspot ya tawi hilo.
Katika risala iliyosomwa kwa mgeni rasmi na Mwenyekiti wa Tawi hilo, Amina Poyo, zimewekwa wazi baadhi ya changamoto mbalimbali zinazolikabili Tawi hilo.
Miongoni mwa changamoto hizo ni kama vile; upungufu wa viti, meza, kompyuta, printa pamoja na mtaji wa kuendeleza vitega uchumi vya wanachama katika kuimarisha Tawi hilo.
Aidha, Poyo ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati ya Kukuza Vipaji na Soka la Vijana ndani ya Klabu ya Simba SC, alitaja mikakati ya kimaendeleo waliyonayo kuwa ni kununua basi dogo na kuchangia ujenzi wa hosteli ya Simba Bunju.
Collins akikata utepe kuashiria kulizindua rasmi tawi la Simba Platnum Supporters SPS.JPG
Comments
Post a Comment