KAMA kuna kituko kilichowaacha hoi mashabiki wa mipasho Jumatatu ya wiki iliyopita, basi ni pale mchezaji wa Yanga, Mbrazil Continho alipoibuka ghafla kwenye onesho la wakongwe wa mipasho, East African Melody na kusakata burudani sambamba na wapenzi wengine.
Kituko hicho kilitokea Jumatatu iliyopita, kwenye ukumbi wa Lango la Jiji, jijini Dar es Salaam, ambapo wana Melody hutumbuiza hapo katika siku siku za Jumatatu.
Continho (katikati pichani) aliyekuwa kavalia pensi ya rangi ya maziwa na mistari meusi huku juu akiwa katinga fulana iliyombana, aliingia ndani ya ukumbi huo majira ya saa 4:30 usiku na kuketi kwenye moja ya viti vilivyotengwa kwa watu maalum.
Ghafla muda si muda, baadhi ya mashabiki walianza kumzunguuka wakimshangaa na wengine kutaka kupiga naye picha, ambapo Continho mwenyewe alitabasamu na kutekeleza matakwa ya mashabiki wake.
Alipoulizwa na mwandishi, Continho alisema kuwa, aliamua kujumuika na mashabiki wa Melody usiku huo, ili kufurahia ushindi walioupata Yanga dhidi ya timu ya Azam FC wa mabao 3-0 kwenye mechi ya Ngao ya Hisani.
Comments
Post a Comment