SAMBA AFUNGIWA MECHI MBILI BAADA YA KUWAONESHEA MASHABIKI KIDOLE CHA KATI...



SAMBA AFUNGIWA MECHI MBILI BAADA YA KUWAONESHEA MASHABIKI KIDOLE CHA KATI...
Christopher Samba alifanyiwa kitendo cha kibaguzi 
BEKI wa zamani wa Queens Park Rangers na Blackburn Rovers, Christopher Samba amefungiwa mechi mbili na chama cha soka cha Urusi (RFU) kufuatia kujibu mapigo kwa kufanyiwa kitendo cha ubaguzi wa rangi.
Beki huyo raia wa Congo, alikuwa anaichezea Dynamo Moscow jana jumapili na alifanyiwa kitendo hicho na mabeki wa Torpedo Moscow. 
Kujibu mapigo, Samba aliwaoneshea kidole cha kati kinachoashiria matusi na alitolewa kipindi cha pili.


Comments