KUNDI kabambe la miondoko ya taarab la Dar Modern Ijumaa usiku lilifanya onyesho maalum la Usiku wa Chai ya Green Label, onyesho lililofana kupita maelezo.
Onyesho hilo limefanyika katika ukumbi wao tulivu ambao nao unaitwa Dar Modern ulioko Magomeni jijini Dar es Salaam.
Watu maalum walioalikwa kwenye onyesho hilo wakapata burudani ya nguvu kutoka kwa Dar Modern Taarab huku pia wakijipatia zawadi kem kem kutoka kwa Chai ya Green Label. Hali kadhalika watu wote waliohudhuria walipata vyakula na vilivyoandamana na kinywaji cha chai ya Green Label.
Dhumuni la onyesho hilo lilikuwa ni kutambuana kati ya Dar Modern na Chai ya Green Label ambao ni wadhamini watarajiwa wa kundi hilo.
Pata picha kadhaa za onyesho hilo.
Mwimbaji Hassan vocha akishambulia jukwaa
Comments
Post a Comment