PHIL NEVILLE ASEMA MAN UNITED INAHITAJI KUTUMIA PAUNI MILIONI 100 ZINGINE KWA USAJILI KABLA HAIJAANZA KUFIKIRIA KITU KINAITWA UBINGWA


PHIL NEVILLE ASEMA MAN UNITED INAHITAJI KUTUMIA PAUNI MILIONI 100 ZINGINE KWA USAJILI KABLA HAIJAANZA KUFIKIRIA KITU KINAITWA UBINGWA

Louis van Gaal splashed out £60m to bring Argentina                  winger Angel di Maria to the club from Real Madrid

BEKI wa zamani wa Manchester United, Phil Neville amesema timu hiyo inahitaji kumwaga pesa nyingine zisizopungua pauni milioni 100 kabla hawajaanza kufikiria kutwaa taji la Ligi Kuu.

Mismu uliopita, United ilimaliza katika nafasi ya saba kwenye msimamo wa Ligi Kuu, hali iliyopelekea kocha mpya Louis van Gaal kufanya 'fujo' za usajili na kutumia pauni milioni 150 kuwanasa Angel di Maria, Luke Shaw, Ander Herrera, Marcos Rojo, Daley Blind na Radamel Falcao aliyechukuliwa kwa mkopo.

Pamoja na hayo United imeshindwa kusajili sentahafu ambapo safu yake ya ulinzi imekuwa ikiyumba msimu huu huku Chris Smalling, Phil Jones na Jonny Evans wakionyesha kiwango duni wakati kinda Tyler Blackett akijaribu kuonyesha uwezo wake.

Neville anaamini bado tatizo halijatatuliwa.

"Najua United imetumia pauni milioni 150", Neville aliiambia BBC Radio 5 Live.

"Nadhani kuna madirisha mawili ya usajili yanakuja ambayo yatahitaji kiasi kama hicho cha pesa – pengine pauni milioni 150 - kabla hawajaanza kufikiria kutwaa taji.

"Kuna maeneo ambayo bado timu inahitaji kuyaziba. Nafikiri sentahafu ni eneo husika zaidi. Eneo la kiungo pia linahitaji kufanyiwa kazi.

"Hakukuwa mabeki wa kati wa kiwango cha kidunia katika dirisha la kiangazi. Ndio maana nadhani madirisha yajayo ya usajili United itasaka beki wa kati wa kiwango cha juu." 



Comments