Bondia anayechipukia kwa kasi issa omar nampepeche au "Peche boy" kama wengi wanavyomwita, ataoneshana umwamba na bondia mkongwe mwenye rekodi nzuri ya kuwapiga kina nasibu ramadhan,majia na kupoteza kwa tabu kwa miyeyusho pia ana historia ya kuwa bondia wa kwanza Tanzania kuwasumbua wafilipino na kucheza mapambano mengi ya ubingwa,nae Issa Omar "peche boy" bondia wa mwananyamala anayejifua katika gym ya bigright boxing, ni kijana mwenye kipaji cha mchezo tangu mdogo na mwenye rekodi ya kushinda mapambano yote 18 huku moja likikosa mshindi.
Issa Nampepeche baada ya kuwapiga kitandula,moro best na juma seleman, inaonekana amekwishaa komaa na sasa anakabiliana na mtihani mwingine mgumu wa juma fundi katika pambano la round nane litakalopigwa siku ya jumamosi tarehe 27/ 9/ 2014 katika ukumbi wa friends kona uliopo manzese huku yakifuatiwa na mapambano mengine ya kina Mohamed Rashid Matumla atayeminyana na Nasibu Ramadhan, Sadiki Momba na Adam Ngange pia kutakuwepo na mchezo mwingine wa kina dada nao ni kati ya lulu kayage atakayezipiga na mtoto wa bondia mkongwe Fatuma Omar yazidu.
Akizungumza na vyanzo vya habari kiongozi wa ngumi na msemaji wa pambano Ibrahim Kamwe alisema "ni kuwa maandalizi ya pambano zima yamekamilika na mabondia wote wapo katika hari nzuri ya mchezo huku dogo issa nampepeche akijiamini zaidi kumshinda juma fundi, na Nasibu Ramadhan akijigamba kulipa kisasi kwa muddy matumla kwa kipigo cha mbwa mwizi,.
Ibrahim kamwe aliongeza kwa kusema kuwa yale malalamiko ya watu kuwa friends corner hotel viti huwa vichache yamefanyiwa kazi na katika pambano hili viti vitakuwa vingi na askari watakuwepo wengi kulinda watu na mali zao na kiingilio kimewekwa kizuri ili watu wenye heshima zao waweze kuja na kufurahia mashindano haya yenye kushirikisha mabingwa vijana wenye vipaji na uwezo wa hali ya juu katika masumbwi
Comments
Post a Comment