PADDY MCNAIR KINDA WA MANCHESTER UNITED ALIYEKUWA NYOTA WA MCHEZO DHIDI YA WEST HAM …azungusha sentahafu ya kufa mtu



PADDY MCNAIR KINDA WA MANCHESTER UNITED ALIYEKUWA NYOTA WA MCHEZO DHIDI YA WEST HAM …azungusha sentahafu ya kufa mtu

Paddy McNair impressed on his United debut and              actually looked more assured than Marcos Rojo

WAKATI kocha Louis Van Gaal akimpanga kinda wa miaka 19 Patrick McNair kama beki wa kati kwenye mechi ya Ligi Kuu dhidi ya West Ham, kila mtu alipigwa na butwaa, lakini baada ya mchezo kumalizika, dogo huyo akajidhihirisha kama nuru mpya kwenye safu ya ulinzi ya Manchester United.

Patrick McNair akawa nyota wa mchezo na kujizolea alama nyingi kuliko mchezaji mwingine yeyote yule. Kwa umri kama wake na kwa mechi yake ya kwanza, tena kwa timu ambayo ipo kwenye shinikizo kubwa, halikuwa jambo la kawaida. United ikashinda 2-1.

McNair akazungusha sentahafu iliyokuwa ikikosekana kwa muda mrefu kwenye ukuta wa United, kiwango alichokionyesha kilikuwa cha hali ya juu na kupelekea hata safu ya kiungo kucheza kwa utulivu.

Patrick McNair raia wa Ireland ya Kaskazini aliyeingia Manchester United akiwa na umri wa miaka 16, alipangwa katika mechi hiyo kufuatia majanga ya kuwepo kwa majeruhi wengi wakiwemo Chris Smalling, Jonny Evans na Phil Jones huku kinda mwingine aliyeanza mechi zote Tyler Blackett akitumikia adhabu ya kadi nyekundu.

Kiuwezo, Patrick McNair akawaacha mbali Chris Smalling, Jonny Evans, Phil Jones na Tyler Blackett. Kama ataendelea na ubora huu aliouonyesha, basi majeruhi hao watajikuta wakisota benchi.

Angalia alama walizopewa wachezaji wote wa Man United na West Ham:

Manchester United (4-1-2-1-2): De Gea 6; Rafael 6, McNair 8, Rojo 6, Shaw 6; Blind 7; Herrera 7 (Valencia 74 6), Di Maria 6 (Thorpe 90 6); Rooney 4; Van Persie 7, Falcao 6 (Fletcher 65 6).

West Ham (4-3-1-2): Adrian 5; Demel 6 (Jenkinson 65 6), Tomkins 6, Reid 5, Cresswell 6; Song 5, Poyet 6, Amalfitano 6 (Cole 61 6); Downing 6: Sakho 7, E Valencia 6



Comments