OGOPA KOPA YA KHADIJA KOPA USO KWA USO NA KING KIKI BAGAMOYO

OGOPA KOPA YA KHADIJA KOPA USO KWA USO NA KING KIKI BAGAMOYO
OGOPA KOPA YA KHADIJA KOPA USO KWA USO NA KING KIKI            BAGAMOYO

KUNDI jipya la muziki wa mwambao Ogopa Kopa linalomilikiwa na malkia wa mipasho Bi Khadija Kopa, limeanza maonyesho yake kimya kimya ambapo Jumamosi hii litakuwa mjini Bagamoyo likiumana jukwaa moja na King Kiki.

Hiyo itakuwa ni ndani ya ukumbi mpya unaokwenda kwa jina la Mageti Mia. Hapa King Kiki na bendi yake ya Wazee Sugu, pale ni Khadija Kopa na Ogopa Kopa …mbona itakuwa raha!

Kundi la Ogopa Kopa ambalo lipo kambini, tayari limekamilisha wimbo mmoja "Mama Mukubwa" utakaoimbwa na Khadija Kopa.

Comments