AMARULA Sauti ya Mola ni mmoja kati ya waimbaji waliotesa sana na bendi ya Diomond Musica International, lakini sasa ameamua kuja na mradi wake binafsi kama msanii wa kujitegemea.
Katika mpango huu, mwimbaji huyu mwenye sauti tamu ameshuka na wimbo "Penzi Langu" hii ikiwa ni katika safari yake ya kuandaa albam yenye jumla ya nyimbo tisa.
"Penzi Langu" imetengenezwa katika studio za Soft Records zilizoko Mwananyamala jijini Dar es Salaam chini ya producer Pitshou Mechant Shemesha.
Pata uhondo hapo chini.
Comments
Post a Comment