MZIGO mpya wa rhumba kutoka mwimbaji Isha Mashauzi uitwao 'Nimlaumu Nani', umetua rasmi kwenye vituo vya radio wikiendi iliyopita na sasa ni wakati wako wa kuusikiliza kupitia Saluti5.
"Nimlaumu Nani" iliyosheni meseji kali ya kimapenzi, imerekodiwa katika Studio za Soft Records zilizopo jijini Dar es Salaam, chini ya produza Pishu Mesha.
Kwa kawaida Isha anafahamika zaidi kwa taarab, lakini kupitia wimbo huu, mwanadada huyu anajitanua zaidi na kuingia kwenye miondoko ya muziki wa dansi.
Baadhi ya wasanii walioshiriki kuunogesha wimbo huo wa dakika tano, ni Kalikiti Moto aliyesimama kwenye kinanda, Rajab Kondo katika gitaa la bass, Pishu Mesha kwenye gitaa la Solo. Sauti zote za uimbaji zinazosikika ndani yake zimewekwa na Isha Mashauzi peke yake.
Ni ngoma nzuri ambayo utapenda kuisikiliza tena na tena.
Usikilize hapo chini.
Comments
Post a Comment