Mzee Kassim Mapili anaendelea na matibabu katika kitengo cha magonjwa ya moyo Muhimbili. Mapili anasema alikuwa anajisikia vibaya na kwenda hospitali ya Mwananyamala wiki iliyopita, na huko alilazwa kisha akafanyiwa vipimo vilivyolazimishwa kulazwa hospitalini hapo, baada ya siku chache akahamishiwa kitengo cha moyo baada ya kuonekana kuwa hali ya si nzuri na inahitaji uangalifu wa ziada. Bahati mbaya katika kulazwa huku, mama yake alipewa habari na kufariki kwa mshtuko, mama yake amezikwa siku ya Jumatano iliyopita na Mzee Mapili hakuweza kuhudhuria msiba wa mama yake ambae mwenyewe anasema alikuwa mzee sana. Kwa wakati huu japo anasema anaendelea vizuri na anashukuru kwa salamu nyingi kutoka kila upande wa Tanzania, lakini bado anahitaji msaada wa hali na mali ili kufuata vizuri matibabu. Kwa wale ambao wangependa kumsaidia Mzee mapili wanaweza kutuma chochote kupitia simu yake ya mkononi 0714486255.
Comments
Post a Comment