MSHINDO JUMANNE SUPER DIRECTOR WA BONGO MOVIES


MSHINDO JUMANNE SUPER DIRECTOR WA BONGO MOVIES

mshindo
NYOTA wa filamu za Kibongo, Mshindo Jumanne ameweka wazi kuwa, amepanga kuhakikisha anaumalizia mwaka huu kwa kufanya mapinduzi mazito katika sanaa hiyo yenye mashabiki wengi kwa sasa.

Mshindo, miongoni mwa Wahariri na Waongozaji mahiri wa muvi, aliyasema hayo jijini Dar es Salaam, katika mazungumzo maalum na mtandao huu, nyumbani kwake, Mgeninani, jijini Dar es Salaam.

Alisema, hivi karibuni ameamua kujitoa kwenye makampuni aliyokuwa akiyatumikia, ili kupata fursa nzuri ya kuendelea kukonga nyoyo za mashabiki wake kupitia kazi atakazozifyatua akiwa na Kampuni
yake ya Safina Movie Shop.

"Nina deni kwa Watanzania, ambapo ili kuhakikisha nalimaliza deni hilo, sina budi kujituma kwenye kuachia filamu zinazoshindana kiwango cha ubora kabla hatujafunga na kufungua mwaka," alisema Mshindo mwenye mafanikio makubwa yaliyotokana na
sanaa hiyo.

Alisema kuwa, hivi sasa yuko mbioni kufyatua kazi mpya inayokwenda kwa jina la 'Uchuro', iliyobeba kisa kizito juu ya athari za kuuendekeza moyo katika mapenzi kwa kumtamani kila unayemuona.



Comments