MSANII WA BONGO FLEVA SIDE BOY MNYAMWEZI AFARIKI DUNIA ...sikiliza wimbo wake "Usimdharau Usiyemjua"


MSANII WA BONGO FLEVA SIDE BOY MNYAMWEZI AFARIKI DUNIA ...sikiliza wimbo wake "Usimdharau Usiyemjua"
MSANII WA BONGO FLEVA SIDE BOY MNYAMWEZI AFARIKI DUNIA            ...sikiliza wimbo wake

MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Saidi Mustafa maarufu kama Side Boy Mnyamwezi (pichani juu) amefariki dunia baada ya kuugua kwa miezi kadhaa.

Mmoja wa marafiki wa msanii huyo, PNC ambaye naye pia ni msanii wa Bongo Fleva ameiambia Saluti5 kuwa Side Boy amefariki katika hospitali ya St Walburg iliyopo Nyangao Lindi.

Bado haijajulikana juu ya taratibu za mazishi ya Side Boy.

Side Boy  aliyekuwa akijiita Rais wa Kusini, alianza kuugua miezi kadhaa iliyopita ambapo Juni 3 mwaka huu, aliandika hivi kwenye ukurasa wake wa facebook: "habari za usiku huu wapendwa! dua zenu zinahitajika sana coz hali yangu c poa kabisaaa".

Miongoni mwa nyimbo zilizompa umaarufu Side Boy ni pamoja "Hujafa Hujaumbika" alomshirikisha Best Nasso na "Usimdharau Usiyemjua" alopewa tafu na Ney wa Mitego.



Comments