MOURINHO AWA MPOLE KWA HISPANIA JUU YA DIEGO COSTA …asema hana jeuri ya kuingilia mipango ya timu ya taifa


MOURINHO AWA MPOLE KWA HISPANIA JUU YA DIEGO COSTA …asema hana jeuri ya kuingilia mipango ya timu ya taifa

Jose Mourinho says he is powerless to prevent                    Spain calling up Diego Costa despite his hamstring                    concerns

JOSE Mourinho amekiri kuwa hana nguvu ya kumzuia mshambuliaji wake Diego Costa kujiunga na timu ya taifa ya Hispania kwaajili ya mechi za kufuzu Euro 2016 mwezi ujao licha ya kuzongwa kwake na majeraha.

Kocha huyo wa Chelsea amekuwa akimpanga Costa kwa tahadhari ya hali ya juu baada ya kurejea kutoka mechi za kimataifa akiwa majeruhi.

Akizungumzia kuhusu uwezekano wa Costa kutajwa kwenye kikosi cha Hispania, Mourinho alisema: "Mimi si lolote katika kufanya maamuzi. Kila kitu kiko wazi. Kila mtu anajua nini kinaendelea kwa Diego. Kila mmoja anajua amekuwa na matatizo kwa muda fulani. Lakini mimi si lolote.

"Inapofika wakati wa timu ya taifa inamhitaji mchezaji wa Chelsea, mimi si lolote. Wanaweza wakawaita wachezaji, kuwatumia au kufanya chochote watakacho. Kiujumla ni nje kabisa ya uwezo wangu. Kitu ninachofikiria na kile ninachohisi havina nafasi yoyote juu ya hilo."



Comments