MASHAUZI TAYARI KWA EID EL HAJI



MASHAUZI TAYARI KWA EID EL HAJI

IMG_0007BAADA ya kufunika kwenye shoo ya Alhamisi iliyopita, ndani ya ukumbi wa Mango Garden, Kinondoni, Ijumaa Kigamboni na Jumamosi Buguruni, Mashauzi Classic sasa inajiandaa kwa ajili ya shamrashamra za Sikukuu ya Eid El Hajj mwishoni mwa  wiki hii.
Meneja wa Mashauzi Classic, Ismail Sumalaga alisema kuwa, Jumapili ya siku ya Sikukuu ya Idd el Hajj, wamepanga kutumbuiza katika ngome yao, Mango Garden, Kinondoni, jijini Dar es Salaam.
Suma alisema kuwa, hiyo imetokana na maombi mengi ya mashabiki wao na ni kwa ajili ya kuwapa burudani kamilifu wakazi wote jijini Dar es Salaam, katika kusheherekea Sikukuu hiyo kubwa duniani kote.
"Kama kawaida ya Mashauzi Classic, tumeandaa sapraizi za nguvu pamoja na burudani za kukata na shoka, ambapo pia tutatambulisha vibao vyetu vipya ambavyo ni maandalizi ya albamu ijayo," alisema Suma.
Mashauzi Classic inayotikisa kwa vibao vyao vingi vikali, inakusanya wasanii wengi mahiri kama vile; Rajab Kondo na Jumanne Boya (Bass), Kalikiti Moto (Kinanda) na Ramadhan Kalenga katika Solo.
Kwa upande wa waimbaji, Mashauzi inajivunia mkali wa sauti anayetamba nchi nzima, Isha Mashauzi, Hashim Said Igwee, Asia Mzinga, Saida Makongo na chipukizi anayetetemesha wakongwe hivi sasa, Thania Msomali.IMG_0008



Comments