WAYNE Rooney amefunga lakini akaambulia kadi nyekundu wakati Manchseter United ikipata ushindi wake wa pili kwenye Ligi Kuu ya England baada ya kuilaza West Ham 2-1 kwenye dimba la Old Trafford.
Baada ya kipigo cha kuduwaza cha 5-3 kutoka kwa Leicester City katika mchezo uliopita, United ikaanza kwa kishindo baada ya Rooney kuandika bao la kwanza dakika ya 2 kufuatia krosi safi kutoka kwa Rafael.
Robin van Persie akaindikia United bao la 2 dakika ya 22 kabla Diafra Sakho kuipatia West Ham bao pekee dakika ya 37.
Katika kipindi cha pili nahodha wa United Wayne Rooney akalambwa kadi nyekundu baada ya kumpiga teke Stewart Downing – rafu ya kijinga inayomfanya mchezaji huyo wa England afungiwe kwa mechi tatu.
Manchester United (4-1-2-1-2): De Gea 6; Rafael 6, McNair 7, Rojo 6, Shaw 6; Blind 7; Herrera 7 (Valencia 74 6), Di Maria 6 (Thorpe 90 6); Rooney 4; Van Persie 7, Falcao 6 (Fletcher 65 6).
West Ham (4-3-1-2): Adrian 5; Demel 6 (Jenkinson 65 6), Tomkins 6, Reid 5, Cresswell 6; Song 5, Poyet 6, Amalfitano 6 (Cole 61 6); Downing 6: Sakho 7, E Valencia 6.
Comments
Post a Comment