MANCHESTER UNITED INGEFUNGWA LEO...WAYNE ROONEY ANGEBEBA MSALABA BAADA YA KUONESHWA KADI NYEKUNDU!




MANCHESTER UNITED INGEFUNGWA LEO...WAYNE ROONEY ANGEBEBA MSALABA BAADA YA KUONESHWA KADI NYEKUNDU!

Mshambuliaji wa Manchester United, Wayne Rooney, katikati akioneshwa kadi nyekundu na mwamuzi Lee Mason
WAYNE Rooney amekuwa shujaa kwa kuifungia Manchester United bao moja katika ushindi wa 2-1 dhidi ya West Ham leo uwanja wa Old Trafford.
Licha ya kazi hiyo nzuri, Rooney alisababisha United icheze ikiwa pungufu kufuatia kuoneshwa kadi nyekundu.
Nahodha huyo wa mashetani wekundu alifunga goli la kuongoza katika dakika ya tano na Robin van Persie aliongeza goli la pili katika dakika ya 22.
Sakho alitumia makosa ya mabeki wa United na kuwafungia wageni goli la kufutia machozi.
Rooney alioneshwa kadi nyekundu baada ya kumfanyia unyama Stewart Downing katika dakika ya 59.
Wayne Rooney akipokea kadi nyekundu ya moja kwa moja baada ya kumfanyia rafu mbaya Stewart Downing wa West Ham

Nahodha wa United, Wayne Rooney akitoka uwanjani baada ya kuoneshwa kadi nyekundu


Comments