INADAIWA Manchester United haitavunja benki ili kumsaji tena nyota wake wa zamani Cristiano Ronaldo hasa baada ya kukataa ofa ya kurudi Old Trafford msimu uliopita.
United chini ya David Moyes ilidhamiria kumsajili Ronaldo lakini badala yake supastaa huyo wa Ureno akasaini mkataba mpya wa kuendelea kukipiga Real Madrid.
Ingawa United ingependa kumrejesha Ronaldo Old Trafford, lakini fungu la pauni milioni 120 kwa mchezaji ambaye anatimiza miaka 30 mwezi Februari, inaonekana ni kubwa sana kwa klabu hiyo tajiri duniani.
United inaamini kama kuna suala la Ronaldo kurejea kwao kiangazi kijacho, basi ni kwa ofa watakayotoa wao na si Real Madrid.
Comments
Post a Comment