MAMA KAWELE KAFANYA MAKUBWA KATIKA FILAMU YA ‘UCHURO’


MAMA KAWELE KAFANYA MAKUBWA KATIKA FILAMU YA 'UCHURO'

Uchuro

NYOTA wa filamu za Kibongo, Grace Mapunda 'Mama Kawele' hivi karibuni anatarajiwa kuanza kuonekana kwenye muvi mpya ya kibongo, inayokwenda kwa jina la 'Uchuro'.

Filamu ya 'Uchuro' inaandaliwa na Kampuni ya Safina Movie Shop, ambayo iko chini ya mwigizaji na mwongozaji mahiri, Mshindo Jumanne.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Mshindo alisema kuwa, katika muvi hiyo, Mama Kawele ataonekana akiwa amecheza nafasi ya mwanamke anayejikuta akichangia mwanaume na mtoto wa kumzaa mwenyewe.

"Kiukweli, katika muvi hiyo, Mama Kawele amejitahidi kucheza katika kiwango cha hali ya juu kabisa, tofauti na picha zote alizowahi kushiriki," alisema Mshindo anayefahamika pia kama 'Superdirector'.

Aidha, Mshindo alisema kuwa, mbali na Mama Kawele, kazi hiyo imekusanya pia nyota wengine wengi wanaotamba hapa nchini kama vile; yeye mwenyewe, Fikiri Salum na Hashim Kambi.





Comments