BEKI wa kulia wa Arsenal Mathieu Debuchy atakuwa nje ya dimba kwa takriban miezi mitatu kufuatia upasuaji wa kiwiko cha mguu, kocha wa Arsene Wenger amethibitisha.
Debuchy aliyesajiliwa dirisha la kiangazi kutoka Newcastle kwa pauni milioni 12, aliumia na kutolewa nje katika mechi dhidi ya Manchester City Septemba 13.
Kulikuwa na matumaini kuwa tatizo si kubwa sana, lakini sasa beki huyo wa Kifaransa atakuwa nje kwa muda mrefu.
Comments
Post a Comment