KAMA mashabiki wa Liverpool walidhani usajili wa kimbunga uliofanywa na timu yao utakuwa na manufaa kuliko msimu uliopita, basi wanapaswa kuchanganua upya fikra zao.
Timu hiyo imeendelea kukutana na vingingi kwenye Ligi Kuu ya England baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 na Everton.
Liverpool wakiwa uwanja wa nyumbani, wakapata bao la kuongoza kupitia kwa nahodha Steven Gerrard kunako dakika ya 67.
Wakati timu hiyo ikiamini imefanikiwa kuokota ushindi mwembamba, Phil Jagielka akaisawazishia Everton katika dakika ya 90.
Liverpool: Mignolet, Manquillo, Lovren, Skrtel, Moreno, Gerrard, Henderson, Markovic, Lallana, Sterling, Balotelli
Everton: Howard, Hibbert, Baines, Jagielka, Stones, Barry, McCarthy, Besic, Mirallas, Naismith, Lukaku
Comments
Post a Comment