FRANK Lampard ameonyesha kuwa umri si tatizo kwake baada ya kutandaza soka bab kubwa kwenye pambano la Capital One kati ya timu yake anayoichezea kwa mkopo Manchester City dhidi ya Sheffield Wednesday.
Katika mchezo huo City ikaangusha karamu ya magoli na kuibugiza Sheffield jumla ya mabao 7-0 huku Lampard akitumbukiza wavuni mipira miwili.
Boss wa City Manuel Pellegrini aliingiza kikosi cha nguvu lakini timu yake ikajikutana ikibanwa katika dakika 45 za mwanzo na kulazimishwa sare hadi kipindi cha kwanza kilipomalizika.
City ambao ni mabingwa watetezi wa Capital One Cup, wakacharuka kipindi cha pili na kudumbukiza mabao manne ya haraka haraka ndani ya dakika 15 za mwazo (Lampard 47, Dzeko 53,Jesús Navas 54,Touré 60).
Dzeko akafunga tena dakika ya 77, kinda Juan Angel Pozo akapachika bao sita dakika ya 88 kabla ya Lampard kuhitimisha karamu ya magoli dakika mbili baadae.
Lampard mwenye umri wa miaka 36 alisajiliwa na New York City ya Marekani dirisha la kingazi kabla haijamtoa kwa mkopo kwa ndugu zao (Man City).
Manchester City (4-1-4-1): Caballero 6, Sagna 7, Demichelis 6, Mangala 6, Kolarov 6.5, Fernandinho 6.5 (Boyata 69, 6), Navas 7.5, Toure 6.5 (Pozo 63, 6), Lampard 7.5, Milner 7.5 (Sinclair 72, 6), Dzeko 6.5.
Sheffield Wednesday (4-1-4-1): Kirkland 6, Buxton 6, Lees 6, Zayatte 6.5, Mattock 6, Coke 6.5 (Dielna 60, 6), Maguire 6.5, Palmer 6 (Helan 69, 6), Maghoma 6.5, May 6.5, Madine 5.5 (Nuhiu 60, 6).
Comments
Post a Comment